Kitengo Cha Mapitio
Kitengo hichi kinahusiana na Mapitio ya Sheria:
- 1.) Kuhakikisha mapendekezo yote ya mapitio ya sheria yanayowasilishwa yanasimamiwa na kutekelezwa.
- 2.) Kubainisha kasoro mbali mbali zilizopo katika sheria na kupendekeza mapitio ya sheria.
- 3.) Kuhakikisha Sheria zilizopo zinakidhi makubaliano ya mikataba ya kimataifa, katiba na misingi ya utawala wa sheria.
- 4.) Kuratibu na kufanyiakazi mapendekezo ya Wizara,, Taasisi,na Wadau wote wa mapitio ya Sheria.
- 5.) Kufanya tathimini ya sheria au aina ya sheria na kushauri iwapo bado zinahitajika.
- 6.) Kuweka sawa marejeo ya sheria kwa Kiswahili na kuziweka katika kitabu kimoja.