Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria namba 16 ya mwaka 1986. Chimbuko hasa la Tume hii ni nia ya Serikali ya kuimarisha Mfumo wa utoaji haki kwa kuhakikisha kwamba Zanzibar inakuwa na Sheria zinazokwenda na wakati.
Aidha ni utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Pius Msekwa iliyoundwa na Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1974 kwa lengo la kufanya mapitio juu ya mfumo wa Mahakama za Tanzania na mwaka 1977 Tume hiyo ilikuja na mapendekezo kadhaa ikiwemo ya kuanzisha Tume ya Kurekebisha Sheria, Kutokana na mapendekezo hayo, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ilipitisha Sheria ya mwaka 1986 iliyoanzisha Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar.
“Kuwa na Sheria zinazokidhi haja kwa maendeleo ya watu wa Zanzibar”
“Kuzirekebisha Sheria za Zanzibar ili zilingane na muelekeo wa mabadiliko na mahitaji ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kwa watu wa Zanzibar.”
"Kujenga uwelewa wa Sheria kwa jamii ili iweze kufahamu haki zao za kisheria na kushiriki katika utafiti wa mapitio ya sheria"