Kitengo Cha Utafiti
Kitengo hichi kimekijikita na tafiti za Kisheria na kina Majukumu haya yafuatayo:
- 1.) Kutafiti sheria kuu mpya na za zamani kutokana na mabadiliko ya sheria husika yaliyofanywa.
- 2.) Kufanya tathimini ya sheria zilizopo na mahitaji yake kulingana na wakati.
- 3.) Kuweka “Database” ya sheria na taarifa zote za utafiti za Tume.
- 4.) Kufuatilia maelekezo na miongozo itakayopelekea marekebisho ya sheria..
- 5.) Kubuni na kushauri njia ya utekelezaji wa sheria husika.
- 6.) Kusimamia uchapishaji wa sheria zilizorekebishwa kwa mpangilio unaokubalika ndani ya vitabu vya sheria.
- 7.) Kusimamia kazi za kurahisisha na kutafsiri sheria katika lugha ya Kiswahili.
- 8.) Kufuatilia maamuzi ya Mahkama za juu, ili kubaini kama kuna maamuzi yanayohitaji kuzingatiwa katika mapitio ya sheria.
- 9.) Kufuatilia miongozo iliyopo ya shughuli za Tume.