SMZ
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar

SMZ

Mapitio yaliyokamilika


Kwa mujibu wa Sheria, Tume ina majukumu ya kufanyia mapitio sheria zote za Zanzibar kwa kuzingatia tafiti, mipango ya kitaifa na mazingira ya Zanzibar na hatimaye kutoa ushauri Serikalini wa sheria husika ili sheria hiyo ilingane na mazingira ya wakati uliopo, baada ya kuchukua maoni kwa wadau na wahusika wengine wa sheria inayopendekezwa. Tume imefanya na kukamilisha mapitio yafuatayo:
Nam. Mapitio/Mapendekezo Maelezo ya Mapitio/Mapendekezo Pakua Ripoti
1. Mapitio ya Sheria ya Utumishi wa Umma Nam. 2 ya 2011 Mapitio hayo yanatokana na kasoro na changamoto zinazogusa utumishi wa umma ambazo zinapaswa kuelezwa wazi ili kuifanya sekta ya utumishi wa umma kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu. Inasubiri
2. Uanzishwaji wa Sheria ya Kusimamia Ukaguzi, Uhasibu na Washauri wa Kodi Zanzibar Mapendekezo hayo yanatokana na ushindani unaoongezeka ulimwenguni kote katika sekta ya fedha kutokana na kuimarika kwa kasi kwa sekta ya teknolojia, ambapo ambapo kwa wateja na raia wanafahamishwa vyema juu ya uchaguzi wa wahasibu, wakaguzi na washauri wa kodi. Inasubiri
3. Uanzishwaji wa Sheria ya huduma Ndogo za Fedha Zanzibar Mapendekezo hayo yanatokana na kukuwa kwa kasi kwa huduma ndogo za Fedha ulimwenguni na kutokuwepo utaratibu mzuri wa kusimamia sekta hizi ili zisiathiri amana zinazowekwa na wananchi. Inasubiri