Kuanzishwa Tume ya Kurekebisha Sheria


Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar

Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria namba 16 ya mwaka 1986. Chimbuko hasa la Tume hii ni nia ya Serikali ya kuimarisha Mfumo wa utoaji haki kwa kuhakikisha kwamba Zanzibar inakuwa na Sheria zinazokwenda na wakati.


Aidha ni utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Pius Msekwa iliyoundwa na Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1974 kwa lengo la kufanya mapitio juu ya mfumo wa Mahakama za Tanzania na mwaka 1977 Tume hiyo ilikuja na mapendekezo kadhaa ikiwemo ya kuanzisha Tume ya Kurekebisha Sheria, Kutokana na mapendekezo hayo, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ilipitisha Sheria ya mwaka 1986 iliyoanzisha Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar.

  • Dira Yetu

    Zanzibar Kuwa na Sheria zinazokidhi haja kwa maendeleo ya watu wa Zanzibar.

  • Lengo Kuu

    Kuzirekebisha Sheria za Zanzibar ili zilingane na muelekeo wa mabadiliko na mahitaji ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kwa watu wa Zanzibar.

  • Dhamira Yetu

    Kujenga uwelewa wa Sheria kwa jamii ili iweze kufahamu haki zao za kisheria na kushiriki katika utafiti wa mapitio ya sheria.

© 2022 LRCZ, Haki zote zimehifadhiwa. Law Review Commission of Zanzibar