Muundo wa Tume ya Kurekebisha Sheria


Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar imeundwa na makamishna sita ambao watano kati yao ni makamishna wa muda na mmoja huteuliwa kuwa Kamishna wa kudumu ambae pia ndie Mwenyekiti wa Tume.

Aidha Tume ina Katibu ambae ndiye ndie mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za Tume. Mwenyekiti, Makamishna na Katibu wa Tume huteuliwa na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majukumu ya Tume ya Kurekebisha Sheria

Majukumu ya msingi ya Tume yameainishwa katika kifungu cha 4 cha Sheria iliyoanzisha Tume hiyo namba 16/1986 ambayo ni pamoja na:-

  • 1. Kupendekeza mabadiliko ya Sheria kwa mujibu wa mazingira ya Zanzibar;
  • 2. Kutafsiri Sheria ikli zifahamike kwa jamii;
  • 3. Kutoa elimu kwa wananchi ili wapate uwelewa wa Sheria hizo;
  • 4. Kushauri njia mpya za utekelezaji wa Sheria;
  • 5. Kuziweka Sheria kwa pamoja;
  • 6. Kuimarisha mashirikiano na Taasisi za nje zenye kazi sawa na Tume;
  • 7. Kuchapisha Makala ya Sheria za nchi za nje ndani ya Zanzibar, ikiwa Makala hayo yanakwenda sambamba na maadili ya Mzanzibari.

Utaratibu wa Kazi na Uwezo wa Tume

  • 1. Tume inaweza kufanya kazi zake kutokana na maelekezo ya Mhe. Waziri mwenye dhamana na masuala ya Sheria ;
  • 2. Maelekezo ya Mwanasheria Mkuu;
  • 3. Tume baada ya kumueleza Mwanasheria Mkuu inaweza kufanya kazi yoyote kwa mujibu wa Sheria hii.;
  • 4. Tume inatakiwa kushirikisha umma katika kufanya kazi zake;
  • 5. Tume inaweza kufanya semina, mahadhara kujadili jambo linalofanyiwa mapitio kwa mujibu wa Sheria hii.

Mambo yanayozingatiwa na Tume katika Kutekeleza Kazi Zake

  • 1. Kuwa na Sheria zinazoendana na Sera mbali mbali za Serikali ;
  • 2. Kutoa mapendekezo ya Sheria yanayozingatia misingi ya Katiba ;
  • 3. Kuwashirikisha wanajamii katika mchakato wa mapitio ya Sheria ;
  • 4.Kushirikiana na Taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali (NGOs) ili kurahisisha kuifikia jamii.;
  • 5.Kukusanya maoni ya jamii kuhusu Sheria inayo rekebishwa.

© 2022 LRCZ, Haki zote zimehifadhiwa. Law Review Commission of Zanzibar