Jumbe Kutoka kwa Mwenyekiti na KatibuNdg. Khadija Shamte Mzee
MWENYEKITI - TUME YA KUREKEBISHA SHERIA - ZANZIBAR

Kwa niaba ya Makamishna na wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria ya Zanzibar, nachukuwa fursa hii ya kukaribisha katika tovuti hii rasmi ya Tume ya kurekebisha Sheria. Tovuti hii imekusudiwa kutoa taarifa muhimu kuhusu uanzishwaji, muundo, mamlaka, matokeo na masuala mengine muhimu kuhusu Tume.Hivyo imani yangu kwamba kupitia tovuti hii utapata taarifa mbali mbali zinazohusiana na kazi za Tume.

Jukumu la msingi la Tume ni kuzirekebisha Sheria za Zanzibar ili zilingane na muelekeo wa mabadiliko na mahitaji ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kwa watu wa Zanzibar.Katika kuhakikisha kwamba jukumu lake linatimizwa Tume ipo tayari kupokea Maoni ambayo yatawasilishwa na wadau kutoka sekta mbali mbali ikiwemo na Sekta Binafsi. Katika suala hili, tunatoa wito kwa wadau wote wasisite kutoa maoni endapo tume ikiwa ipo katika kufanya mapitio ya sheria.

Mwisho kabisa, nawashukuru wadau na washiriki ambao wamekuwa wakiiunga mkono Tume na kushiriki kwa ukarimu katika shughuli za Tume.Ndg. Mussa Kombo Bakari
KATIBU - TUME YA KUREKEBISHA SHERIA - ZANZIBAR

Ninafuraha kuwajuulisha wadau wa Sheria na jamii Kwa ujumla kupitia tovuti hii rasmi ya Tume itatumika kama kituo ama nyenzo muhimu katika kutoa taarifa mbali mbali za kazi za Tume ikiwemo, Ripoti za Mapitio na Tafiti Mbali Mbali za Sheria, Jarida na vipindi mbali mbali vinavyoendeshwa katika Televisheni vilivyoandaliwa na Tume.

Ni dhamira yetu katika kutekeleza Majukumu ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Zanzibar kuwa na Sheriazinazokidhi haja kwa maendeleo ya watu wa Zanzibar. Hivyo tunaishajihisha Jamii kwa Ujumla ikiwemo na sekta mbali mbali kujitokeza katika utoaji wa maoni wa Sheria ambazo tunaendelea kuzipitia.

Vile vile unaweza kutumia tovuti hii kwa kuwasiliana nasi moja kwa moja kwa kutuma maoni yako kupitia barua pepe inayotumika na Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar.

Natanguliza Shukurani zangu za dhati na kwa niaba ya Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar kwa Ujumla.


WASHIRIKI WA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA

© 2022 LRCZ, Haki zote zimehifadhiwa. Law Review Commission of Zanzibar